Kujitoa
ufahamu! Ndivyo alivyofanya Mtangazaji Lulu Semangongo ‘Aunt Lulu’ baada ya kukutwa
akifanya vitendo vya kifuska hadharani bila tone la aibu. Mtangazaji
huyo alikutwa akifanya uchafu kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Mbezi-Beach
jijini Dar alipokuwa amejumuika na mastaa wa Kundi la Scorpion Girls, Isabela
Mpanda, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuzi’
ambapo alikuwa akinywa vinywaji vikali na kuvuta sigara. Timu yetu ya
Operesheni Fichuo Maovu (OFM) ilimshuhudia Aunt Lulu akiwa amelewa bwii huku
akimkatia mauno mwanaume mmoja bila kujali wingi wa watu waliokuwa eneo hilo.
OFM
walimrekodi video Aunt Lulu ambaye muda wote alikuwa akizungumza maneno
yalioshiria kuzidiwa na kilevi kichwani. Ukiacha ulevi wa sigara na pombe,
mwanadada huyo alitia fora baada ya kumgeukia mwanaume huyo aliyekuwa naye
kisha kufanya naye mambo ya chumbani hadharani hivyo kusababisha wenye aibu zao
kutazama pembeni.
Baada
ya kufanikiwa kumrekodi video na kushindwa kuzungumza naye kutokana na hali
hiyo ya ulevi, siku iliyofuata mwandishi wetu alimtafuta Aunt Lulu ili kumuhoji
sababu ya kujiachia na kutouthamini mwili wake kwa kuvuta sigara na kunywa
pombe kali lakini hakupokea simu siku nzima. Gazeti hili linaendelea kumtafuta
atakapopatikana atabanwa ili kujua kama kuna kitu kinamsibu hadi aamue kunywa pombe
na kuvuta sigara kiasi cha kufanya vitendo vya aibu hadharani.
Post a Comment