Rapper Chemical amedai kauli yake ya kuwa yeye bado ni bikira (bado
hajaupoteza usichana wake) umewafanya wanaume wengi kumtokea huku watu
wengine wakijitokeza na kutaka kumtafutia mwanaume.
Chemical amedai wakati anatoa kauli hiyo hakudhamiria kuweka wazi
suala hilo lakini alilazimika kutoa jibu hilo baada ya kuulizwa swali.
“Kiukweli toka nimefanya vile napata comment nyingi sana wengine
wanasema sikuwa na busara kufanya vile,” Chemical alikiambia kipindi cha
FNL cha EATV. “Lakini nataka kuwaambia kwanza sikujitangaza ila
ilitokea tu baada ya kuulizwa vitu ambavyo inawezekana siwezi kuvijibu,”
Aliongeza, “Lakini napenda kuwaonyesha watu tusilazimishe kwa kuwa
wewe umepitia kitu fulani wote tunatakiwa kuwa tumepitia jambo hilo,
mimi najua background yangu niliyotokea siku zote na focus kwenye
‘Career’ yangu sitaki kitu chochote kiniharibie hasa sijui mwanaume ajae
kuniharibia maisha yangu” alisema Chemical
Mbali na hilo Chemical aliweka wazi juu ya watu ambao wamekuwa
wakijitokeza kutaka kumtafutia mwanaume na kusema yeye hana shida hata
wakimtafutia mwisho wa siku yeye lazima ampime kuona kama anamfaa au
hafai.
Post a Comment