Kuelekea mchezo wa leo kati ya Man United na Liverpool watavaa jezi
maalum zilizoandikwa “Seeing is Believing” (Kuona ni kuamini) ikiwa ni
kutoa sapoti ya kuongeza uelewa wa kampeni ya kuzuia upofu na uharibifu
wa uwezo wa kuona.
Liverpool wataungana na wadhamini wao Standard Chartered wanafanya
hivyo zikiwa zimepita siku 4 tangu kuazimishwa kwa “World Sight Day”
ambayo huazimishwa kila mwaka kwa lengo la kuleta ufahamu juu ya upofu
na uharibifu wa uwezo wa kuona.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ” nikiwa kama mtu ninayevaa
miwani ,ninafahamu kuona ni muhimu katika maisha yangu .kwa hiyo hili
suala ni muhimu sana kwangu.”
Miwani ya Klopp itapigwa mnada baada ya mchezo ili kuchangia pesa
katika kampeni hiyo, na jezi za wachezaji za mechi hiyo, pamoja na
kitambaa cha unahodha pia vitauzwa kwa ajili ya kuongeza fedha za
kusaidia kampeni hiyo.
Post a Comment